Afisa Afya kata Nyasubi Mkola Vedastus (27) mkazi wa Nyahanga wilayani Kahama akiwa katika kituo cha afya cha Igalilimi Kahama |
Afisa
Afya kata Nyasubi Mkola Vedastus (27) mkazi wa Nyahanga wilayani Kahama
mkoani
Shinyanga amenusurika kufa kwa kuunguzwa vibaya sehemu mbalimbali za
mwili wake ikiwemo sehemu za siri baada ya kumwagiwa maji ya maharage
yaliyokuwa yanatokota jikoni na shemeji
yake(mke wa kaka yake) Anna Makula anayedaiwa kuwa na uhusiano naye wa
kimapenzi.
Akizungumza
na wandishi wa Habari Vedastus waliomtembelea katika kituo cha Afya cha
Igalilimi mjini Kahama alipolazwa akipatiwa matibabu amesema tukio hilo
limetokea juzi saa kumi jioni wakati anatoka bafuni ndipo shemeji yake
alipomwagia maji hayo ya maharage.
Vedastus
amesema alimwagiwa maji ya maharage yaliyokuwa jikoni yakichemshwa na mke wa kaka yake bi Anna Makula wakati akitoka bafuni
kuoga na wakati huo alikuwa amevaa kaushi na taulo.
Amedai kuwa chanzo cha tukio hilo
alikuwa na ugomvi wa ndani na shemeji yake ambaye wamepanga nyumba moja katika
mtaa huo.
Amesema wakati anakwenda bafuni kuoga alimpita shemeji yake
pembeni ya mlango akiongeza maji kwenye maharage wakati huo huo chumbani kwake akiwa
amemwacha rafiki yake wa kike ambaye ana mahusiano naye kimapenzi na wakati anarudi
ndani ndipo alijikuta akimwagiwa maji hayo na shemeji yake.
Baadhi
ya watu waliozungumza na Malunde1 blog wanasema tukio hilo linahusishwa
na mahusiano ya kimapenzi baina ya Anna Makula na Mkola Vedastus wote
wakiwa ni wakazi wa mtaa mmoja na wakiwa wamepanga nyumba moja huku
wakiishi kama familia moja.
"Hawa
wamepanga nyumba moja,huyu afisa hajaoa,kila mtu ana chumba chake
inavyoonekana shemeji aliona wivu baada ya kuona kuna mwanamke ndani ya
chumba cha shemeji yake ambaye ana mahusiano ya kimapenzi,hii ni hatari
sana huyu jamaa alikuwa anafanya mapenzi na mke wa kaka yake",wameeleza
mashuhuda hao.
Kwa
upande wake mmiliki wa kituo cha Igalilimi Dkt.Shija Luis amesema hali ya
mgonjwa ni mbaya hasa kutokana na Afisa huyo kuunguzwa vibaya sehemu mbalimbali
za mwili wake ikiwa ni pamoja na sehemu za siri hivyo itachukua muda mrefu
kumfanyia uchunguzi wa kina kwani ajali ya moto ni mbaya sana.
“Mara
nyingi moto unasababisha maji kupungua sana
maana joto kali la moto bado linaendelea kufukuta ndani kwa ndani ili
kumnusuru ni kumwongezea dripu nyingi za maji na hivyo inatuwia vigumu kutoa
taarifa za kidaktari mapema,majibu yatapatikana ndani ya siku tatu na kama ataendelea vibaya tutamhamishia
hospitali ya Wilaya”,amesema Dk.Luis.
Naye
kaimu mganga mkuu wa hospitali ya mji wa Kahama Deo Nyaga alipoulizwa kuhusiana
tukio hilo amesema hana taarifa zozote zinazomhusu afisa wake.
Hata
hivyo kaka wa Vedastus akijibu maswali ya wanahabari waliofika katika kituo
hicho alikiri kutokea kwa hali hiyo katika familia yake ana kusema wamepanga
nyumba moja na mdogo wake na wanaishi kama familia moja na kinachoendelea kati
ya mkewe pamoja na mdogo wake katika tukio hilo alipigiwa simu na majirani na hajui chochote kuhusu kilichotokea.
source; malunde blog.
No comments
Post a Comment