Sunday, 17 May 2015

Rais Morsi ameridhia hukumu ya kifo, asema yuko tayari kunyongwa


Duru za kuaminika nchini Misri zimeripoti kuwa Muhammad Morsi, rais wa nchi huyo aliyeondolewa madarakani na jeshi amesema hana pingamizi yoyote na hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi yake na mahakama ya jinai ya Cairo. Mtandao wa habari wa Alyaumus sabi'i ulioko karibu na serikali ya Cairo umeripoti kuwa wakati akirejeshwa jela ya Burj al Arab baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi yake kuhusiana na kesi ya kutoroka jela ya Wadin Natrun, Morsi alisisitiza kwamba yeye ni rais halali wa Misri, na kwa sababu hiyo hatokata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa na mahakama ya mwanzo. Mahakama ya jinai ya Cairo jana ilitoa hukumu ya kifo dhidi ya Muhammad Morsi na zaidi ya watu wengine mia moja wakiwemo viongozi na wanachama wa harakati ya Ikhwanul Muslimin na kuiwasilisha hukumu hiyo kwa Mufti Mkuu wa nchi hiyo. Hukumu hiyo imelalamikiwa na kupingwa vikali ndani na nje ya Misri. Radiamali ya karibuni kimataifa imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye mbali na kulaani hukumu hiyo amewataka viongozi wa Misri kutochukua hatua ambayo itadhoofisha amani, uthabiti na utawala wa sheria katika eneo. Ban aidha amesema anafuatilia kwa makini mwenendo wa matukio hayo yanayojiri nchini Misri. Wakati huohuo Usama Morsi, mtoto wa kiume wa Morsi amesema hukumu hiyo ya mahakama ya jinai ni sehemu ya vita vya kinafsi na kisiasa vya utawala wa wafanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Mapinduzi ya wananchi wa Misri na shakhsia wa mapinduzi hayo, na kuongeza kuwa wafuasi wa Ikhwanul Muslimin wameanzisha harakati dhidi ya hukumu hiyo, muhimu zaidi ikiwa ni kuendeleza wimbi la mapinduzi kwa lengo la kufuta hukumu hizo batili. Usama Morsi amesisitiza kwamba katika siku zijazo Misri itashuhudia matukio ya kushangaza
tehran swahili radio mei 17

No comments

Post a Comment