Hali nchini Burundi bado ni tete huku mapigano makali yakiendelea kuripotiwa kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Pierre Nkurunziza na wale wanaomuunga mkono Jenerali Godefroid Niyombara aliyetangaza kuipindua serikali ya Bujumbura siku ya Jumatano. Kuna habari za kutatanisha kuhusu aliko rais Nkurunziza. Kiongozi huyo ameandika kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter kwamba amerudi nchini Burundi na kwamba bado serikali yake iko imara. Hata hivyo, kiongozi huyo bado hajaonekana hadharani. Naibu kiongozi wa mapinduzi, Jenerali Cyrille Ndayirukiye, amekiri kufeli mapinduzi hayo. "Kwa mtazamo wangu nadhani harakati zetuzimeshindwa kwani tumekabiliwa na nguvu kubwa ya jeshi linaloungamkono serikali ya sasa" amesema Ndayirukiye. Kuna habari kwamba jeshi tiifu kwa Nkurunziza limefanikiwa kuchukua udhibiti wa uwanja wa ndege wa Bujumbura pamoja na kituo cha redio na televisheni cha taifa ingawa upande wa upinzani umekanusha habari hizo.
Huku hayo yakijiri, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani jaribio la mapinduzi nchini Burundi lakini pia limemkosoa Rais Nkurunziza kwa kuitumbukiza nchi katika lindi la machafuko kutokana na tangazo lake la kugombea tena muhula wa tatu.
iran Swahili radio, mei 15
No comments
Post a Comment