Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta wamejadiliana leo kuhusu njia za kukabiliana na kitisho cha
wanamgambo wa itikadi kali wa kundi la Al Shabab waliohusika na mauaji
ya watu 148 katika chuo kikuu mjini Garissa mwezi uliopita.Kerry
aliyewasili Nairobi jana Jumapili pia amewakumbuka wahanga wa
mashambulizi ya mabomu dhidi ya ubalozi wa Marekani ya mwaka 1998 mjini
Nairobi ambapo zaidi ya watu 200 waliuwawa. Hivi punde waziri huyo wa
mambo ya nje wa Marekani akizungumza katika mkutano na waandishi
Marekani sambamba na nchi nyingine za Magharibi zinatoa mafunzo na
msaada mwingine kwa vikosi vya usalama vya Kenya.Mwezi uliopita waziri
wa mambo ya nje wa Kenya Amina Mohammed alisema nchi yake inahitaji
msaada zaidi wa kijaasusi na hatua za kiusalama kutoka Marekani na
washirika wake barani Ulaya kuzuia mashambulizi zaidi ya al Shabab.
Monday, 4 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment