Friday, 8 May 2015

HALI YAW TETE MAFURIKO KILA KONA.

MVUA kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia juzi, imesababisha mafuriko na kuua watu watatu, kuharibu nyumba kadhaa na miundombinu y... thumbnail 1 summary
Mkazi wa Jangwani, Dar es Salaam, Oscar Albert akionesha namna mafuriko yalivyoathiri makazi yake kufuatia mvua zilizonyesha jijini jana. (Picha na Fadhili Akida).MVUA kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia juzi, imesababisha mafuriko na kuua watu watatu, kuharibu nyumba kadhaa na miundombinu ya barabara na maji katika sehemu mbalimbali.
Nyumba nyingi zilizingirwa na maji, barabara hazikupitika kwa urahisi na kulikuwa na adha kubwa ya usafiri. Gazeti hili lilipotembelea maeneo mbalimbali, lilishuhudia maji yakiwa yametanda kila kona, kuanzia kwenye makazi ya watu hadi barabara kuu.
Madaraja yalikuwa yamezidiwa na maji na barabara ya Morogoro ilifungwa kwa muda baada ya maji kupita juu ya daraja. Katika maeneo ya Yombo Dovya, Kigogo, Buguruni Kwa Mnyamani, Msasani Bonde la Mpunga, Mikocheni, Vingunguti, Tabata Kisiwani na Jangwani, hali ilikuwa mbaya zaidi, kwani mito iliacha mkondo wake na maji kuvamia makazi ya watu.
Baadhi ya nyumba, kuta zake zilibomoka, huku nyingine zilifunikwa na maji. Hali ilikuwa mbaya hata makao makuu ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), ambayo ofisi zake zilizingirwa na maji na kusababisha wageni waliokwenda katika ofisi hizo, kuvua viatu na kutembea majini ili kuweza kufikia ofisi husika.
Katika eneo la Kigogo, baadhi ya watu walionekana wakisafirisha vifaa vya nyumbani baada ya kuchafuka na matope. Watu hao walieleza kuwa matope hayo yalitokana na maji yaliyoingia ndani ya nyumba zao usiku wa kuamkia jana, huku kuta za nyumba zao zikiwa zimebomoka.
Huko Jangwani maji yalizingira kila upande, ikiwa ni pamoja na sehemu kulipojengwa kituo cha mabasi yaendayo kasi, nyumba za maeneo hayo hadi uwanja wa mpira wa Klabu ya Soka ya Yanga.
Katika maeneo hayo ya Jangwani, gazeti hili lilishuhudia watu wakiwa wamekaa kando ya barabara wakiwa na vyombo vya ndani ikiwemo makochi na vitanda. Wengine waliweka vyombo vya jikoni juu ya bati za nyumba. SOURCE HABARI LEO

No comments

Post a Comment