Wed May 20 2015
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS, MART NOOIJ
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania TAIFA STARS, MART NOI amesema
bao la mapema waliofungwa na Swaziland katika mchezo wa kwanza wa
michuano ya COSAFA liliwachanganya wachezaji na kucheza kwa shinikizo
kubwa kwa muda wote wa mchezo.
Bao la SWAZILAND katika mchezo huo limefungwa na SIFISO MABILA kwa shuti kali katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza.
STARS ilipoteza nafasi zaidi ya tano kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake SAIMON MSUVA na nahodha JOHN BOCCO ambao walishindwa kukwamisha mpira wavuni.
TAIFA STARS itatupa karata yake ya pili kwa kuikabili MADAGASCAR siku ya JUMATANO katika uwanja wa ROYAL BAFOKENG, katika mchezo wake wa kwanza, MADAGASCAR imeibuka na ushidi wa mabao MAWILI kwa Moja dhidi ya LESOTHO.
No comments
Post a Comment