mei 5, 2015
Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea Jumatano kwa mchezo
mmoja utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,
wenyeji timu ya Azam FC watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo
msimu huu, timu ya Young Africans.
Mechi hiyo itachezeshwa na
mwamuzi wa kati Jacob Adongo kutoka Mara, akisaidiwa na washika
vibendera Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma (Dar es Salaam), huku
mwamuzi wa akiba akiwa ni Hussein Kalindo (Dsm) na Kamisaa wa mchezo huo
ni Damian Mabena kutoka Tanga.Hata hivyo, kwa Yanga, itakuwa ni kama kukamilisha ratiba wakati Azam wanahitaji ushindi katika vita yao ya Simba ya kugombania nafasi ya pili.
Bingwa, ambao ni Yanga watawaikilisha nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa afrika wakati mshindi wa pili (kati ya Azam na Simba) wataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho.
No comments
Post a Comment