Polisi nchini Israel wakiwa juu ya
Farasi wamekabiliana na waandamanaji kutoka makundi ya Wayahudi wenye
asili ya Ethiopia ambao wanadai kubaguliwa na Polisi wa taifa hilo.
Katika
maandamano hayo yalitokea Tel Aviv, Polisi walitumia mabomu ya machozi
na maguruneti kuwatawanya mamia ya waandamanaji hao. Watu kadhaa
wamejeruhiwa wakiwemo maafisa wa Polisi 20. Wayahudi wenye asili ya
Ethiopia waliitisha maandamano kufuatia picha za video zilizosamabaa
wiki iliyopita ambazo zinaonyesha askari wenye sare wenye asili ya
Ethioppia wakiteswa na Polisi. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
ametoa wito kurejesha hali ya Amani na kuahidi kuwa polisi watafuatilia
tuhuma hizo na kuzifanyia uchunguzi wa kina
Sunday, 3 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment