Kwa muujibu wa madereva hao, kupitia kwa kiongozi wao, Rashid Said aliwatangazia madereva hao kuwa mgomo huo utaendelea hadi hapo Waziri Mkuu Pinda atakapofika kuongea nao.
“Tutakaa hapa hapa. Hadi hapo Waziri Mkuu Pinda atakapokuja kuongea na sisi. Kama hatofika basi mgomo huu utakuwa endelevu hadi muafaka ufike!!” alieleza Rashid Saidi huku akishangiliwa kwa nguvu kubwa na madeeva hao.
Kwa sasa eneo la Ubungo miuondombinu ni mibomu huku maji machaafu ya mvua yakizagaa hovyo, ambapo baadhi yao wameendelea kulalamikia Serikali kuwa inakusanya kodi zao za bure ikiwemo ushuru huku kituo kikiwa kichafu ambapo poia wamebainisha kuwa, wameambiwa waziri Mkuu hawezi kufika kwenye kituo hicho kutokana na kuwa ni pachafu.
Kauli hiyo ya kudaiwa mahala hapo ni pachafu ndio maana waziri Mkuu anashindwa kufika, imechukuliwa kwa hisia tofauti na madereva hao huku kila mmoja akishindwa kuamini kama imetolewa na Pinda ama ni msaidizi wa Pinda.
Kwa upande wake mmoja wa viongozi wa madereva hao, maarufu kama BONGE, ambaye amekuwa akikubalika sana na madereva hao alipanda juu ya jukwaa na kisha kuwatangazia madereva wenzake kuwa, Mgomo huo utaendelea bila kikomo hata ukiwa wa siku tatu, watakula biskuti na siku itaenda.
“MADEREVA! TUPO PAMOJA. TUTAKAA HAPA HADI PINDA AFIKE. NA ASIPOFIKA TUNAO UWEZO WA KUKAA HAPA BILA KUFANYA KAZI NA TUKASHINDIA BISKUTI!! SI TUNAWEZA!!!” aliuliza na kuitikiwa kwa shangwe na madereva wenzake. NDIOO NDIO HAPA HATOKI KIONGOZI YOYOTE WA KWENDA KWA WAZIRI PINDA, TUTAKAA HAPA HAPA HADI KIELEWEKE! WALISEMA MADEREVA HAO.
Hata hivyo, licha ya mgomo wa Mwezi Aprili mwaka huu kuwa na msululu wa magari ya Polisi na viongozi wao pamoja na viongozi wa Serikali, lakini kwa siku ya leo hakuna kiongozi hata mmoja wa Kitaifa ama wa Serikali aliyefika kuongea na madereva haao.
MABANGO Yaliyobebelewa na baadhi ya waandamanaji yalionyesha kauli tata ambayo rais Kikwete alikutana nayo siku ya mei mosi kutoka kwa walimu ikisema SHEMEJI UNATUACHAJE, ambapo imebadilishwa na kuwa MADEREVA UNATUACHAJE ?
Ila kwa nje, umati mkubwa wa watu wakiwemo wasafiri na wapita njia wakiendelea kusubiria hali ya mgomo, gaari za Polisi zimetaanda kila mahala, ambapo majira ya saa 5 asubuhi, Polisi walipiga bomu moja la machozi katika eneo la Ubungo maji ambaapo kulikuwa na hali ya kutoelewana ya tafrani na kuisha.
No comments
Post a Comment