Wednesday, 6 May 2015

Madiwani wa KALIUA waadhimia kuzuia chakula kutoka wilayani mwao

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya KALIUA mkoani TABORA limeazimia kuzuia chakula kutoka nje ya wilaya hiyo bila kibali maalum ... thumbnail 1 summary
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya KALIUA mkoani TABORA limeazimia kuzuia chakula kutoka nje ya wilaya hiyo bila kibali maalum cha kufanya hivyo.

Madiwani hao wamesema kuna kila dalili ya maeneo mengi kukosa chakula kutokana na mvua hafifu zilizonyesha msimu huu katika wilaya hiyo, hivyo wanapaswa kuchukua tahadhari ili kuepukana na tatizo la njaa.

Kutokana na hoja hiyo, Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya KALIUA IBRAHIMU amewataka Madiwani kusimamia hali ya chakula katika maeneo yao badala ya kulalamika.

No comments

Post a Comment