Thursday, 7 May 2015

Mamia ya miili katika milima ya Nepal

Viungo vya mwili vimetapakaa katika maeneo ya mlima mmoja nchini Nepal, wakati watu karibu 300, wengi wao raia wa kigeni, wakiaminika kufuki... thumbnail 1 summary
Viungo vya mwili vimetapakaa katika maeneo ya mlima mmoja nchini Nepal, wakati watu karibu 300, wengi wao raia wa kigeni, wakiaminika kufukiwa katika eneo hilo na theluji iliyoporomoka kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mwezi uliopita. Afisa wa serikali katika maeneo hayo amesema waokoaji wameondoa miili sita kutoka kijiji cha Langtang, kaskazini mwa mji mkuu Kathmandu, lakini operesheni zao zinaathiriwa na hali mbaya ya hewa. Karibu miili 100 ilipatikana katika sehemu hiyo ya mlima mwishoni mwa wiki. Serikali ilisema watu 7,759 waliuawa katika tetemeko hilo la ardhi la Aprili 25 na zaidi ya 16,000 wakajeruhiwa.

No comments

Post a Comment