Wednesday, 6 May 2015

MANNY PACQUIAO ashitakiwa nchini MAREKANI

Wed May 06 2015 Bondia MANNY PACQUIAO KATIKA masumbwi Bondia MANNY PACQUIAO ameshitakiwa katika mahakama ya wilaya ya NEVADA k... thumbnail 1 summary
Wed May 06 2015


Bondia MANNY PACQUIAO
KATIKA masumbwi Bondia MANNY PACQUIAO ameshitakiwa katika mahakama ya wilaya ya NEVADA kwa kosa la kutosema ukweli juu ya kuumia kwake bega kabla ya pambano lake dhidi ya FLOYD MAYWEATHER JUNIOR lililochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Watu wawili ambao majina yao hayajawekwa hadharani wamefungua kesi dhidi ya PAQUIAO wakimtuhumu bondia huyo kuwahadaa wanunuaji wa tiketi za pambano hilo, watazamani wa televisheni na wacheza kamari kwa kushindwa kwake kutoa taarifa mapema za kuumia kwake bega kabla ya mchezo huo.

PAQUIAO pia anaweza kuwa matatani zaidi na KAMISHENI YA WANAMICHEZO NEVADA kutokana na kudanganya katika fomu yake ya afya kabla ya pambano hilo.

Katika fomu ya dodoso la maswali ya afya aliyopewa PAQUIAO na kuijaza, aliweka alama ya hapana katika kipengele cha iwapo anamaumivu ya bega, viwiko vya mikono au mikono na hivyo kuonekana wazi kuwa amedanganya.

Iwapo akikutwa na hatia PAQUIAO atafungiwa kutojihusisha na masumbwi katika kipindi cha mwaka mmoja hadi miaka MINNE na kulimwa faini ya dola elfu Tano za marekani.

Katika hatua nyingine wakati hayo yakitokea FLOYD MAYWEATHER amekubali kurudiana na PAQUIAO ndani ya mwaka mmoja kutoka sasa.

Kwa mujibu na taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari vya MAREKANI, MAYWEATHER ameripotiwa akisema kuwa yupo tayari kurudiana na PAQUIAO pindi atakapopona bega lake baada ya kufanyiwa upasuaji.

Kauli hii ya MAYWEATHER inapingana na kauli yake ya mwanzo aliyoitoa baada ya pambano lake na PAQUIAO kuwa atastaafu ngumi baada ya pambano lake la mwezi SEPTEMBA mwaka huu

No comments

Post a Comment