Waziri
wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry,amesema kwamba amekuwa
na mazungumzo ya kirafiki kuhusiana na mzozo wa Ukraine pamoja na mambo
mengine na mwenyeji wake rais wa Urusi , Vladimir Putin, katika ghuba ya
bahari ya shamu pwani ya Sochi.
Lakini pia Kerry alikutana na
waziri wa masuala ya mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, katika
ziara yake ya kwanza tangu mgogoro wa Ukraine ulipoanza mwaka wa jana.Kerry pia hakusita kuzungumzia masuala ya ziada ambayo yalijiri katika mazungumzo yao kwamba ni juu ya yanaoendelea baina ya Iran na Syria. Amesema kwamba ni muhimu kuzingatia makubaliano waliyofikia baina ya Marekani na Urusi wakati wakiangazia masuala mengine yanayo ikabili dunia.
Mapema kabla ya kuanza mazungumzo hayo, waziri huyo ma mambo ya nchi za nje wa Marekani, alipata fursa ya kuweka shada la maua katika makaburi ya askari waliopigana vita vikuu vya pili vya dunia mjini Sochi. Uhusiano baina ya Urusi na Marekani umeshuka kwa kasi baada ya Urusi kujihusisha harakati za krimea na kuwaunga mkono wapiganaji wa waasi walioko upande wa Mashariki mwa Ukraine
BBC
No comments
Post a Comment