Thursday, 14 May 2015

Mataifa mbalimbali yalaani jaribio la kumuondoa Rais NKURUZINZA

   Fri May 15 2015 Baraza la usalama la umoja wa Afrika Mataifa na Taasisi mbalimbali duniani wametoa tamko la kulaani kile ... thumbnail 1 summary
  
Fri May 15 2015
Baraza la usalama la umoja wa Afrika
Mataifa na Taasisi mbalimbali duniani wametoa tamko la kulaani kile kinachodaiwa kuwa ni jaribio la kutaka kumuondoa madarakani Rais wa BURUNDI - PIERRE NKURUNZIZA.

Katika taarifa zao MAREKANI na Umoja wa Mataifa wametaka pande zinazovutana nchini BURUNDI kuvumiliana na kutafuta njia bora ya kumaliza mgogoro uliopo na si kwa njia ya mapinduzi.

Tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya NKURUNZIZA lilitolewa na Meja Jenerali GODEFROID NIYOMBARE kwa madai kuwa hakubaliani na uamuzi wa kiongozi huyo kuwania nafasi ya Urais kwa Muhula wa Tatu.

Kumekuwa na habari za kutatanisha kuhusiana na tukio hilo, huku maafisa wa serikali ya BURUNDI wakisema kuwa jaribio la kumpindua Rais NKURUNZIZA limeshindwa na kwamba vikosi vinavyomtii vinaendelea kuyalinda maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na makazi ya kiongozi huyo na kituo cha Redio na Televisheni cha Taifa.

Habari zaidi zinadai kuwa Maafisa wa serikali ya BURUNDI wameliambia Shirika la Utangazaji la UINGEREZA – BBC kuwa Rais NKURUNZIZA aliyekua akihudhuria Kikao cha Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini TANZANIA ameshindwa kurejea nchini mwake baada ya ndege iliyombeba kushindwa kutua nchini humo.
tbc may 15...

No comments

Post a Comment