Monday, 4 May 2015

Mazungumzo ya Taliban na serikali yaendelea Qatar

Taarifa kutoka Qatar zinasema kwamba wajumbe wa  kundi la Taliban wamekutana na viongozi wa kisiasa wa Afghanistan kwa siku ya pili nchi... thumbnail 1 summary
Taarifa kutoka Qatar zinasema kwamba wajumbe wa  kundi la Taliban wamekutana na viongozi wa kisiasa wa Afghanistan kwa siku ya pili nchini Qatar jana na pande hizo mbili zimejadiliana juu ya uwezekano wa kuwepo usitishaji mapigano lakini zimeshindwa kukubaliana kuhusu hatua ya kuendelea kuwepo wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.Taarifa hizo zimedokezwa na mmoja wa washiriki kwenye mkutano huo.Mazungumzo hayo ya faragha yaliyonuiwa kumaliza uasi ambao umeigubika Afghanistan tangu wanajeshi wanaoungwa mkono na Marekani kuliondosha kundi la Taliban madarakani mwaka 2001.Mazungumzo hayo ambayo sio rasmi yanayosimamiwa na wizara ya mambo ya nje ya Qatar  yamekuja katika wakati ambapo mapigano yameongezeka baada  ya kuondoka kwa wanajeshi wengi wa Marekani na vikosi washirika nchini humo.Kundi la Taliban hivi karibuni lilianzisha mashambulizi kaskazini mwa nchi hiyo ambapo wapiganaji wake waliingia kwenye vitongoji vya mji wa Kunduz mji mkuu wa mkoa huo wa Kaskazini.

No comments

Post a Comment