Wafalme wa nchi za Ghuba wamekutana Jumanne (05.05.2015) kwa mkutano uliohudhuriwa pia na Rais Francois Hollande wa Ufaransa wakati wasiwasi wa jumuiya ya kimataifa ukizidi kuongezeka kuhusiana na vita nchini Yemen.
Baraza la Ushirikiano la Ghuba la nchi sita za Kiarabu za Kisunni linakutana Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia wakati eneo lao likikabiliwa pia na tishio la wapiganaji wa jihadi huku kukiwa na wasi wasi wa kufikiwa kwa makubaliano ya mwisho ya nyuklia na Iran.
Nchi hizo zina wasi wasi kwamba taifa la Kishia la Iran yumkini bado likawa na uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia chini ya makubaliano ambayo yatapunguza uwezo wake wa kinyuklia ili iondolewe vikwazo vya kimataifa vyenye kuathiri vibaya uchumi wa nchi hiyo.
Kabla ya Hollande kiongozi mwengine pekee wa kigeni aliyewahi kualikwa katika mkutano wa kilele wa baraza hilo la GCC katika historia yake ya miaka 34 ni Mahmoud Ahmadinajad wakati huo akiwa rais wa Iran mwaka 2007.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry atawasili Riyadh kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo hapo kesho na Alhamisi. Marekani imekuwa ikishinikiza kusitishwa kwa mapigano nchini Yemen kwa misingi ya kibinaadamu ili kuwezesha misaada inayohitajika mno ya chakula, mafuta na mahitaji ya kibinaadamu ifikishwe katika maeneo inakohitajika.

No comments
Post a Comment