Diwani
wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimsaidia Waziri wa
maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupanda kingo za mto,
alipotembelea mto Ruvuma mpakani na Msumbiji kutoa kifutajasho kwa watu
waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.
Diwani
wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimwongoza Waziri
wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipotembelea mto Ruvuma katika
kijiji cha Manyuli wilayani Masasi, mpakani na Msumbiji alikokwenda
kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto
huo.
Waziri
wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa
Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine
kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani
kwake.
Wanakijiji
wa Manyuli, wilayani Masasi wakimsikiliza Waziri wa maliasili na
Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumza nao jana, alitembelea watu
waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta
machozi kutoka wizarani kwake.
Waziri
wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikabidhi hundi ya fidia kwa
Katibu Tawala wilaya ya Masasi Dunford Peter ili zigawiwe kwa watu
walioathiriwa na mamba katika vijiji vilivyo kando ya mto Ruvuma jana,
ikiwa ni mpango wa serikali kufidia watu waliojeruhiwa ama kuuawa na
mamba nchini.
No comments
Post a Comment