Thursday, 7 May 2015

Ofisi ya RC yavunja gofu kwa mil. 100/-

OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kubaini kiasi cha... thumbnail 1 summary
Modestus Kilufi OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), kubaini kiasi cha Sh milioni 96.6 kimetumika kubomoa jengo bovu mali ya ofisi hiyo, ili kupisha ujenzi wa ofisi mpya za mkuu wa mkoa huo.
Hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam, mbele ya Kamati hiyo wakati Ofisi hiyo ikipitia ripoti ya ukaguzi wa hesabu kutoka kwa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha 2012/13.
Wakati kamati hiyo ikifanya mapitia hayo, CAG alibaini matumizi makubwa ya fedha zilizotumika kwa ajili ya kubomoa jengo bovu, lililoko jirani na ofisi za Wilaya ya Temeke ili kupisha ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa huo, kutokana na ofisi hizo kwa sasa kuwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara eneo la Ilala.
Akihoji matumizi ya fedha hizo, mjumbe wa kamati hiyo, Modestus Kilufi alimuomba mwenyekiti wa kamati hiyo kwa jana Gaudence Kayombo kumwagiza CAG, kupitia hesabu hizo, ili kubaini matumizi yake, kwani ni fedha nyingi zilizotumika kwenye kazi hiyo.

No comments

Post a Comment