Tue May 05 2015
SERENA WILLIAMS afuzu hatua ya 3 michuano ya wazi HISPANIA
Kwenye teniss mchezaji namba moja kwa ubora wa teniss duniani
upande wa kinadada SERENA WILLIAMS amefuzu kwa hatua ya tatu ya michuano
ya wazi ya MADRID nchini HISPANIA baada ya kupata ushindi mwepesi dhidi
ya SLOANE STEPHENS.
SERENA alipata ushindi wa seti mbili kwa bila kwa matokeo ya 6-4 na 6-0 dhidi ya mmarekani mwenzake SLOANE na kuweka rekodi ya kushina michezo 22 mfululizo mwaka huu.
SERENA ambaye ni bingwa wa mataji makubwa ya teniss 19 duniani hajawahi kupoteza mchezo wowote ule wa kimashindano tangu mwaka 2010.
No comments
Post a Comment