Friday, 22 May 2015

Sheria iwashughulikie waliotajwa na CAG

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),... thumbnail 1 summary

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amewasilisha ripoti ya tano za ukaguzi wa fedha kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2014 akibainisha ufisadi wa zaidi ya Sh600 bilioni katika maeneo mbalimbali na matumizi ya fedha ambayo hayana maelezo ya kutosha.

Hii ni ripoti ya kwanza ya Profesa Mussa Assad aliyepokea kijiti hicho kutoka kwa Ludovick Utouh, aliyestaafu kwa mujibu wa sheria za ajira serikalini tangu Novemba 5, 2014. Ripoti ya Profesa Assad inatokana na ukaguzi uliofanywa katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na ufanisi wa maeneo mbalimbali.

Ripoti hizo zinaonyesha jinsi watumishi hewa wa umma wanavyoendelea kulipwa mishahara, wakiwamo wastaafu, misamaha ya kodi na ukiukwaji wa ununuzi na matumizi yasiyoeleweka ya fedha katika Wizara ya Ujenzi na Kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu na ufisadi Tanesco.

Kasoro hizi kwenye ripoti hiyo siyo ngeni, hata CAG aliyepita, Ludovick Utouh, naye kila mwaka wa fedha wa Serikali alikuwa akibainisha kasoro hizo na ripoti yake ya mwisho iliibuka na kashfa ya uchotwaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Watanzania wamekuwa wakilia kutaka Serikali itumie sheria zake kukomesha ufisadi huu, wabunge ndani ya Bunge wamekuwa wakilia, wengine wakizungumza hadi kupata hasira wakiilaumu Serikali kutoifanyia kazi ripoti ya CAG.

No comments

Post a Comment