Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Simon Msuva amerejea nchini Tanzania akitokea nchini Afrika ya Kusini alipokwenda kufanya majaribio kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.
Msuva aliripotiwa kutoroka kuelekea nchini humo kufanya majaribio katika klabu inayoshiriki ligi kuu ya Bidvest Wits.Msuva, ambaye ameiwezesha Yanga kuwa mabingwa akiwa mfungaji bora baada ya kupashika mabao 17, ameiomba Yanga kumkubalia kujiunga na timu hiyo endapo atafuzu jaribio lake baada ya kurejea kwake siku Jumapili.
Habari zinasema kuwa mabosi wa Bidvest wameridhishwa na mchezaji huyo na wanafungua milango ya mazungumzo na timu yake ya Yanga ili kumsajili kwa gharama yoyote.
No comments
Post a Comment