Wakuu
nchini Nepal sasa wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana
na tetemeko jingine jipya lililotokea nchini humo, imepanda na kufikia
zaidi ya watu 40.
Mamia ya watu walikimbilia usalama wao katika barabara za mji mkuu Kathmandu.Mji wa Namche Bazaar, karibu na mlima Everest umeshuhudia maafa makubwa.
Tetemeko hilo kubwa lililosikika hadi nchini India, lilisababisha vifo vya watu watatu huko.
Tetemeko la awali lililotokea tarehe 25 Aprili , lilisajili vipimo vya 7.8.
Madhara ya tetemeko hili hayajabainika ila inasemekana kuwa lilitikisa mji mkuu wa India New Delhi, vilevile mji mkuu wa Bangladesh Dhaka.
bbc,
No comments
Post a Comment