dalili hizo zilijitokeza hadharani juzi kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Majengo, Moshi akimtaja Dk Slaa kama ndiye rais ajaye huku akieleza uwezekano wa Ukawa kuchukua nchi.
Moshi. Kuna kila dalili kwamba Chadema na vyama washirika vina mpango wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kugombea urais Oktoba mwaka huu.
Moshi. Kuna kila dalili kwamba Chadema na vyama washirika vina mpango wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kugombea urais Oktoba mwaka huu.
Dalili hizo zilijitokeza hadharani juzi kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Majengo, Moshi akimtaja Dk Slaa kama ndiye rais ajaye huku akieleza uwezekano wa Ukawa kuchukua nchi.
Lissu alimtaja Dk Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kuwa ndiyo wabunge wa Chadema ambao hawajawahi kushindwa na CCM tangu mwaka 1995.
“Historia hiyo itasema mbunge mmoja kati yao (ambao hawajawahi kushindwa na CCM) ni Mzee Ndesamburo na historia hiyo itasema mbunge wa pili ambaye hajawahi kushindwa na CCM ni Dk Willibrod Slaa, rais wetu ajaye,” alisema Lissu.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema, alisema katika historia ya Taifa hili kuna uwezekano mkubwa wa Chadema na vyama washirika kuingia Ikulu baada ya Oktoba.
Vyama washirika ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimepanga kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote za uchaguzi kuanzia urais hadi udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Dk Slaa aligombea urais 2010 na kushika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 2.3 sawa na asilimia 26.34 nyuma ya Rais Jakaya Kikwete aliyeshinda kwa kura milioni 5.3 sawa na asilimia 61.17.
Hadi sasa Ukawa haijateua wagombea wake katika ngazi hizo ambazo ni urais, ubunge na udiwani ambao watachuana na wagombea wa vyama vingine.
Katika mkutano
Katika hotuba yake hiyo, Lissu alisema: “Katika miaka 20 ya kwanza ya mfumo wa vyama vingi, kuna wabunge wawili pekee ambao hawajawahi kushindwa na CCM.”
Kauli hiyo ya Lissu iliwafanya wananchi hao kulipuka kwa furaha na kukatisha hotuba hiyo.
Hata hivyo, Lissu hakufafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo zaidi ya kusisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kuenzi mchango wa kiongozi huyo na wa Ndesamburo. mwananchi
No comments
Post a Comment