Umoja wa Afrika waonya kuhusu uchaguzi wa Burundi
Umoja wa Afrika umeonya leo kuwa hali nchini Burundi siyo nzuri kwa maandalizi ya uchaguzi, ikisema haingeweza kuwatuma waangalizi wa uchag...
Umoja wa Afrika umeonya leo kuwa hali nchini Burundi siyo nzuri kwa maandalizi ya uchaguzi, ikisema haingeweza kuwatuma waangalizi wa uchaguzi baada ya kuzuka maandamano makali yaliyochochewa na uamuzi wa rais wa nchi hiyo kugombea muhula wa tatu. Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika Bibi Nkosazana Dlamini -Zuma ameiambia televisheni ya China - CCTV kuwa kando na mahakama ya katiba ya Burundi, ufafanuzi wote unaojitokeza kisheria ni kuwa hapastahili kuwepo muhula wa tatu. Takribani watu 15 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa tangu mwishoni mwa mwezi wa Aprili, baada ya chama tawala cha CNDD-FDD kumteua Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu hali iliyozusha maandamano ya kila siku. Hii leo watu watatu wameuawa na wengine kadhaa wamajeruhiwa katika makabiliano mapya, baada ya Rais Nkurunziza kusisitiza kuwa atagombea kwa muhula wa tatu ambao utakuwa wake wa mwisho ikiwa atachaguliwa. Zaidi ya wakimbizi 35,000 wa Burundi wamekimbilia nchi jirani za Rwanda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
No comments
Post a Comment