Wanasayansi wanasema kuwa kufanya
kazi katika muda usio wa kawaida kikazi au katika mazingira yaliyo ya
upweke kunaweza kuzeesha ubongo na kufanya uwezo wa utendaji kuwa duni.
Utafiti
huo umeeleza katika jarida la Occupational and Environmental Medicine
kuwa iwapo kazi za kupokezana, mfano nyakati za usiku zitafanywa kwa
takriban miaka kumi mfululizo zitazeesha ubongo kabla ya wakati wake.Wanasayansi wanasema ahueni imeonekana kwa watu baada ya kuacha kufanya kazi hizo lakini ilichukua miaka mitano kurejea kwenye hali ya kawaida.
Utafiti huu unaelezwa kuwa muhimu, kwa kuwa waathiriwa wengi kutokana na tatizo hilo wamekuwa wakilala usingizi wa mang'amung'amu.
Wataalam hawa wameiambia BBC kuwa miili na akili zimejengwa kwa kufanya kazi mchana na kulala nyakati za usiku.
Athari mbaya ambazo zinaelezwa kutokana na mtindo huo wa ufanyaji kazi ni madhara ya Saratani na uzito mkubwa.
Timu ya wanasayansi kutoka chuo cha Swansea na Toulouse wameonesha kuwa kuna madhara ya kiakili pia.
No comments
Post a Comment