Wednesday, 13 May 2015

Uongozi wa Vatican watambua rasmi nchi ya Palestina

Vatican imeitambua rasmi nchi ya Palestina katika katika ... thumbnail 1 summary

Vatican imeitambua rasmi nchi ya Palestina katika katika sera zake mpya.
Kwa mujibu wa sera hizo mpya zilizokamilishwa leo Jumatano, Ofisi ya Papa (Holy See) imebadilisha uhusiano wake wa kidiplomasia kutoka uhusiano wa Vatican na Chama cha Ukombozi wa Palestina PLO na kuwa uhusiano wa Vatican na nchi ya Palestina.
Tarehe 29 Novemba 2012, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio la kupandishwa hadhi ya Palestina katika umoja huo kutoka "mshiriki mtazamaji asiye na utambulisho" kuwa "nchi shiriki mtazamaji" licha ya utawala wa Kizayuni wa Israel kupinga vikali suala hilo.
Vatican ilipongeza hatua hiyo ya wanachama 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Hatua ya hivi sasa ya Vatican ya kuitambua rasmi nchi ya Palestina imechukuliwa wakati ambapo Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas anatarajiwa kuonana na Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, siku chache zijazo yaani Mei 16, huko Vatican.
tehran swahili radio.

No comments

Post a Comment