Hata hivyo, vijana hao wa Chadema ambao baadaye walikusanyika katika
ukumbi wa Hoteli ya Corridor Springs, walisema walikubaliana na Lema
kwamba wapewe malipo yao ya maandamano kila baada ya kazi, lakini mara
zote mbunge huyo alikuwa akiwahadaa na kwamba madai yalipokuwa mengi,
Lema aliwakumbusha kuwa wako katika kuipigania nchi na hivyo huo ulikuwa
ndio mchango wao kwenye harakati.
ZAIDI ya vijana 1,000 wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini hapa, wameandamana kupinga hatua ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye pia ni kiongozi wa chama hicho, kutaka kugombea tena uwakilishi wa jimbo hilo.
Vijana hao walioongozwa na aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani hapa, Rashid Shubert Mbakizao ambaye pia aliwahi kuwa dereva, mlinzi na mshauri wa Mbunge Lema kabla hawajahitilafiana katika masuala kadha, likiwemo lile la kutowalipa ujira stahiki vijana waliokuwa wanakusanywa mitaani ili waandamane na kufanya fujo mjini.
“Mimi nilikuwa na kazi ya kuwakusanya madereva wa bodaboda, vijana wasio na kazi pamoja na akinamama ili tuandamane kwa sababu yoyote ile ambayo mbunge wetu angetutangazia, lengo likiwa ni kuwatisha viongozi wa serikali na wafanyabiashara hapa mjini kuwa yeye ana nguvu kubwa na hivyo wawe tayari kufanya chochote atakachowaagiza,” alibainisha Mbakizao.
No comments
Post a Comment