Serikali ya Burundi imewaagiza waandamanaji katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura kusitisha maandamano yao dhidi ya hatua ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Mamlaka imewapatia waandamanaji hao saa 48 kuondoa vizuizi walivyoweka katika barabara za mji huo.Hakuna maandamano yanayoendelea leo kufuatia vifo vya waandamanaji wawili lakini waandalizi wake wamesema kuwa maandamano yataendelea siku ya jumapili.
Waandalizi wanasema kuwa bwana Nkurunziza anakiuka katiba kwa kuwania muhula wa tatu,lakini mapema wiki hii mahakama ya kikatiba nchini Burundi iliamua kuwa rais Nkurunziza ana haki ya kuwania muhula wa tatu.
Takriban watu 18 wameuawa tangu maandamano hayo yaanze wiki mbili zilizopita. BBC MEI 9
No comments
Post a Comment