Mon May 18 2015
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa MWANZA CHARLES MKUMBO
Jeshi la Polisi Mkoani MWANZA limewaagiza waganga wa jadi wilayani SENGEREMA mkoani humo kujisajili rasmi katika mamlaka zinazohusika ili kuwabaini waganga wanaoendesha shughuli zao kinyume na utaratibu. Akizungumzia hatua hiyo katika mkutano na waganga wa jadi wilayani SENGEREMA, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa MWANZA CHARLES MKUMBO, amesema hatua hiyo inalenga kukabilina na mauaji ya watu wenye ualbino pamoja na Vikongwe, ambapo kati ya waganga wa jadi 1622 , ni waganga 164 pekee ambao wamesajiliwa wilayani SENGEREMA.
Afisa Maliasili wilaya ya SENGEREMA, PAUL PONTIANI amesema idara hiyo itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria waganga wa jadi ambao watapatikana na nyara za serikali ambazo huzitumia katika shughuli zao za uganga ikiwemo ngozi, kucha, meno ama mifupa ya wanyamapori.
No comments
Post a Comment