Fri May 22 2015
Mratibu wa Zoezi la Uandikishaji wa Wananchi katika Daftari la Wapiga Kura mkoa wa Mbeya CONSTANTINE MUSHI
Mratibu wa Zoezi la Uandikishaji wa Wananchi katika Daftari la Wapiga Kura mkoa wa Mbeya CONSTANTINE MUSHI, amewahakikishia wananchi wote mkoani humo kwamba waondoa mashaka wote wataandikishwa kama ilivyopangwa. MUSHI ametoa kauli hiyo wakati akitembelea baadhi ya Vituo vya kujiandikisha na kukutana na changamoto ya Mashine za BVR kusuasua na kukwamisha zoezi hilo linalosubiriwa na wananchi wengi mkoani Mbeya.
Wananchi wameonesha muitikio chanya katika kujitokeza na kuandikishwa katika daftari la wapiga kura huku serikali ya Mkoa wa Mbeya ikisema iko karibu na wananchi kuhakikisha wote wenye sifa ya kujiandikisha wanaandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kama ilivyopangwa.
No comments
Post a Comment