Wanaobeza mwenge wa uhuru watakiwa kupuuzwa
Watanzania wameaswa kuwapuuza watu wote wanaoubeza Mwenge wa Uhuru kwa kudai kuwa hauna manufaa yoyote kwa Watanzania. Rai hiyo imetolewa na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji Safi ya Bomba katika Kijiji cha MINGOYO katika Manispaa ya LINDI.
Akiongea na wananchi wa Mingoyo KARIM HARUM MZEE amesema Haiwezekani kutenganisha Mwenge wa Uhuru na Historia ya Tanzania kabla na baada ya Uhuru wa nchi
Akizungumzia mradi wa Maji wa Mingoyo KARIM MZEE amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha Vijiji vyote hapa nchini vinapatiwa Maji safi ya Bomba ili kuondokana na tatizo la Maji na hivyo kuwawezesha wananchi kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Ukiwa Manispaa ya Lindi Mwenge wa Uhuru Umekimbizwa jumla ya kilometa 178, umeweka Mawe ya msingi miradi Mitatu, Umefungua Mradi mmoja na Kuzindua Miradi Minne yenye thamani ya Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mbili na Milioni Mia Sita Sitini na Tisa.
tbc mei 15-2015.
No comments
Post a Comment