Takriban watu 10 wameuawa katika shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga katika msikiti mmoja wa Shia mkoa wa mashariki wa taifa la Saudi Arabia ,kulingana na daktari mmoja.
Daktari wa kukabiliana na dharura katika hospitali ya Qatif amesema kuwa takriban watu sabini wamejeruhiwa huku wengine wakijeruhiwa vibaya.Walioshuhudia wameripoti mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali uliopo katika kijiji cha al-Qadeeh,katika jimbo la Qatif.
Ni kisa cha kwanza cha aina hiyo kutokea Saudi Arabia huku kukiwa na mvutano katika eneo hilo kati ya waislamu wa madhehebu ya Sunni na Shia.
Kundi la Islamic State limedaiwa kutekeleza shambulizi kama hilo katika taifa jirani la Yemen siku ya ijumaa ambalo liliwajeruhiwa watu kadhaa.
Hatahivyo halijatoa tamko lolote kuhusu shambulizi la bomu mashariki mwa Saudia na hakuna kundi jingine lolote lililojihusisha na shambulizi hilo.
Picha za runinga ya kundi la Hezbolla al-Manar zilionyesha vioo vilivyovunjika pamoja na vifusi ndani ya msikiti.
Miili iliozibwa na nguo ilionekana imetapakaa katika sakafu ya msikiti huo.
Watu wa dhehebu la Shia walio wachache wanaishi mkoa wa mashariki na kumekuwa na malalamishi ya washia wanaotaka kupewa haki zaidi.
Hili ni shambulizi la kwanza lililotekelezwa katika msikiti wa Shia.
Tukio hilo linajiri huku muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendeleza kampeni yake dhidi ya waasi wa kishia katika taifa jirani la Yemen.
Taifa la Saudi Arabia pia limetishwa na Islamic state ambalo linalengwa na muungano wa kimataifa iwemo ufalme huo wa kisunni.
No comments
Post a Comment