Wavuvi kutoka Indonesia wamesema kuwa wameamriwa na Serikali kuwa wasiwalete wahamiaji wanaopatikana wakielea kwenye vyombo baharini wasiokuwa na chakula au maji ya kutosha.
Maelfu ya wahamiaji wanadhaniwa kuwa wanaelea Baharini katika maeneo karibu na Indonesia, Thailand na Malaysia.Ni wale watu wanaojitahidi kufika nchi kavu pekee wanaoruhusiwa katika nchi hizo.
Watu wengi wanataka taifa la Myanmar kuchukua wajibu mkubwa zaidi kuhusiana na wahamiaji hao lakini taifa hilo limekataa likidai kuwa halipaswi kulaumiwa kwa hali hiyo.
No comments
Post a Comment