Sunday, 10 May 2015

WAZIRI MKUU ATOA TAMKO JUU YA BOOM; SPECIAL FACULTY KUINGIZWA LEO.

Wazir mkuu akiendelea kutoa maelezo ya kina juu ya masuala yenye ukakasi Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma, Kitivo cha Sanaa z... thumbnail 1 summary
Wazir mkuu akiendelea kutoa maelezo ya kina juu ya masuala yenye ukakasi
Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dodoma, Kitivo cha Sanaa za lugha na sayansi ya jamii (social & humanities) imeweka wazi juu ya masuala ambayo yamekuwa ni mafumbo kwa wanachuo wengi chuoni hapa. Akizungumza na Tegemeo la Wote, Mh. Burchard Wilibroad (waziri mkuu) katika siku ya Jumapili tarehe 9 aliweka wazi juu ya suala la pesa ya special faculty ambayo ilisainiwa wiki mbili zilizopita kuwa kwa taarifa alizonazo pesa hiyo itaingizwa siku ya leo ambayo ni Jumatatu au Jumanne kwa kuwa hata cheki yake imeshatoka Benki tayari.
kwa upande mwingine Waziri mkuu aliendelea kutoa msimamo juu ya pesa za malazi (BOOM), na kusema, "Boom bado ni tatizo kwa vyuo vyote nchini, na bodi wanadai kuwa hata wao hawajapata pesa kutoka hazina, hivyo ni namna ambayo tunajitaidi kuendelea kufuatilia kwa ukaribu ili pesa zitakapofika basi zifanyiwe mchakato wa haraka na kuingizwa mapema, lakini majina bado hayajatoka bodi".
akitoa msimamo wa serikali alisema, "nafikiri ni vyema tuwafikie bodi uso kwa uso huku tukijiandaa na utaratibu mwingine wa kuweza kujua zaidi, na tumeshazianza hatua hizo na sasa tunasubiri ndani ya wiki hii tukifanya mchakato kidogokidogo halafu tutaendelea kujuzana ikishindikana zaidi tutawasikiliza wanachuo wanasemaje (yaani nguvu na maamuzi ya umma)".
Wakati huohuo alipoulizwa kuhusu tatizo la maji alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa mabomba yaliyo mengi na mifumo yake kwa ujumla katika visima ni mibovu, lakini siyo sababu ya kuwaumiza raia, alisema "hata kama ndiyo hivyo sidhani kuwa mfumo mbovu wa miundombinu unaweza kuwa kikwazo maana tuna mafundi wa Chuo na ni suala tu la kuwafuata na kuja kurekebisha, hili naliona na kesho mida ya kazi ofisini ntakua nao bega kwa bega tena hata niwalete ili washuhudie ubovu wa huduma zao juu ya maji"
Pia waziri mkuu aliulizwa swali la hatima ya UDOSO hii na Nyingine mpya na akafunguka kusema kuwa UDOSO ya sasa bunge lake litavunjwa siku ya jumatano ili kupisha mchakato wa uchaguzi wa serikali mpya ya wanafunzi 2015/2016.
Waziri mkuu alimalizia kusema, "kwa kweli ni vyema hata mtusaidie katika kusambaza matangazo na kwenye mitandao ya kijamii, maana sasa haya tunayobandika njiani watu hata hawayaoni hivyo kutumia hata hii mitandao ya kijamii ni jambo zuri nafikiri muendelee kuwahabarisha katika habari mbalimbali na zenye uhakika.
baada ya mahojiano.

ENDELEA KUWA NASI KWA HABARI ZAIDI.

.............mshirikishe na mwenzako..........

 wasiliana nasi kwa habari na matangazo kupitia blog yetu au wasiliana moja kwa mo

ja 0673-042061.

 

No comments

Post a Comment