Maafisa
nchini Pakstan wanasema kuwa watu 43 wameuawa katika shambulizi
lliliofanywa ndani ya basi lililokuwa limewabeba waislamu wa asili ya
kishia katika mji mkubwa wa Karachi.
Maafisa wanasema watu wengine kumi na watatu walijeruhiwa.Polisi wanashuku kuwa shambuliz hilo limetekelezwa na kundi la wasuni wenye msimamo mkali.
Basi hilo lilikuwa limewabeba watu sitini kutoka katika jamii ya waislamu wa kishia walio wachache nchini Pakistan.
Maafisa wanasema kuwa watu sita waliokuwa na bunduki kwenye pikipiki walilazimisha basi hilo kusimama.
Waliingia katika basi hilo na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Wengi waliouawa ni wanawake na watoto.
Baada ya mashambulizi hayo washambuliaji hao wanasemekana kutoweka kwa urahisi.
Mkuu wa polisi mkoani humo Ghulam Haider Jamali amesma huenda shambulizi hilo lilifanywa na kundi linaloshikilia itikadi kali lililokuwa limepigwa marufuku.
Hivi majuzi lilihusika vile vile kuwapiga risasi maafisa wakuu wa polisi huko Karachi.
Picha za video za shambulizi hilo zinaonesha basi lililo na mashimo mengi likivuja damu.
bbc
No comments
Post a Comment