Monday, 18 May 2015

Afrika Kusini yawaondoa wahamiaji haramu 5,645

       Serikali ya Afrika Kusini imewarudisha nyumbani wahamiaji haramu 5,645 tangu mashambulizi yaliyotokana na chuki dhidi ya raia wa kige... thumbnail 1 summary
Afrika Kusini yawaondoa wahamiaji haramu 5,645      Serikali ya Afrika Kusini imewarudisha nyumbani wahamiaji haramu 5,645 tangu mashambulizi yaliyotokana na chuki dhidi ya raia wa kigeni yamalizike mwishoni mwa mwezi Aprili. Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais Jeff Radebe amesema wageni hao ni wale walioamua kuondoka kwa hiari.
Kati ya raia hao kulikuwa na Wamalawi 3,506, Wazimbabwe 1,440, Wamsumbiji 682, na Watanzania 17. Halikadhalika kufuatia hujuma za hivi karibuni dhidi ya raia wa kigeni, takribani wahamiaji 1000 walipata ushauri nasaha. Aidha Wizara ya maendeleo ya jamii ya Afrika Kusini inawasaidia wageni waliopoteza makazi yao katika vurugu hizo. Mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya raia wa kigeni katika miji mikubwa ya Afrika Kusini kama Johannesburg na Durban, yalisababisha vifo vya watu wasiopungua saba huku wengine wengi wakijeruhiwa na biashara zao kuporwa.
Mashambulizi dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini yaliongezeka kufuatia matamshi ya Mfalme wa kabila la Zulu, Goodwill Zwelithini, aliyewataka wageni kuondoka nchini humo.

No comments

Post a Comment