Monday, 18 May 2015

Kanisa Katoliki DRC lakosoa ukandamizaji wa polisi

       Kanisa Katoliki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekosoa vikali ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na v... thumbnail 1 summary
Kanisa Katoliki DRC lakosoa ukandamizaji wa polisi       Kanisa Katoliki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limekosoa vikali ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya polisi nchini humo dhidi ya wahajiri. Taarifa ya Kanisa Katoliki imeeleza kuwa, wahajiri haramu wanaoishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekuwa wakikandamizwa vibaya na vikosi vya polisi vya nchi hiyo hatua ambayo ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu. 
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, polisi wamekuwa wakiwadhalilisha na kuwatesa wahajiri haramu nchini humo na kukiuka wazi haki zao za kimsingi. Kanisa hilo limesema, kamatakamata kubwa inayoendeshwa na vikosi vya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakinzana na sheria za kimataifa.
Ripoti zinaonesha kuwa, wiki hii pekee wahajiri 600 wametiwa mbaroni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

No comments

Post a Comment