Afrika
Kusini imeanzisha operesheni ya kuwafurusha raia wa mataifa mengine ya
Afrika kufuatia vurumai za kibaguzi zilizoibuka dhidi ya wageni katika
taifa hilo hivi majuzi.
Zaidi ya wageni 400 kutoka Msumbiji walikuwa katika kundi la kwanza kufukuzwa.Afrika Kusini imechukua hatua hiyo baada ya vurumai ya kibaguzi dhidi ya wageni iliyopelekea watu saba raia wa kigeni kuuawa na wenyeji waliokuwa wakilalama kuwa wamechukua nafasi zao za kazi.
Mapigano hayo ya kibaguzi yalitibuka katika miji ya Durban na Johannesburg wenyeji walipoanza kuwavamia wageni pamoja na kuwapora mali yao.
Serikali ya Msumbiji imeshangazwa na hatua hiyo ya kuwaondoa raia wake kwa nguvu huku waziri wake wa maswala ya kigeni Oldemiro Baloi akisema alikuwa anatarajia kufanya mazungumzo na mwenzake wa Afrika Kusini.
Waziri huo alisema haelewi kwa nini raia wa Msumbiji wanakamatwa na kuondolewa nchini humo kwa nguvu ilhali swala hilo lilikuwa linashughulikiwa baina ya serikali hizo mbili.
Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko huko anasema hatua hii ya serikali imewashangaza wengi hususan baada ya serikali kupewa ilani ya mahakama dhidi ya kuwakamata na kuwafukuza wageni.
No comments
Post a Comment