Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ametoa ...
09:37
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen ametoa mwito wa
kuongezewa muda usimamishaji vita wa siku tano kwa ajili ya masuala ya
kibinadamu. "Ninaziomba pande zote kuongeza muda wa kuheshimu
makubaliano hayo kwa uchache kwa siku tano zaidi," amesema mjumbe
maalumu wa Umoja wa Mataifa nchni Yemen Bw. Ismail Ould Sheikh Ahmed.
Mjumbe huyo ametoa mwito huo leo ambayo ni siku ya mwisho wa kile
kilichodaiwa kuwa ni makubaliano ya kusimamisha vita yaliyoanza Mei 12.
Madai hayo ya kusimamisha vita kwa muda wa siku tano yamekuja baada ya
takriban wiki saba tangu Saudi Arabia ilipoanza mashambulizi ya pande
zote dhidi ya wananchi wa Yemen tena bila ya idhini ya Umoja wa Mataifa.
Hata hivyo Saudi Arabia imeshindwa kufanikisha lengo angalau moja la
kuivamia Yemen huku harakati ya Ansarullah, jeshi na wananchi wa Yemen
wakiendelea kudhibiti mikoa yote mikubwa kama ambavyo pia riyadhi
imeshindwa kumrejesha madarakani Abd Rabbuh Mansur Hadi, Rais wa Yemen
aliyejiuzulu na kukimbilia Saudia. Hii ni katika hali ambayo licha ya
Saudia kudai kusimamisha vita huko Yemen, lakini mashambulizi yake
hayajasita na kila leo inaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo
tofauti ya nchi hiyo ya Kiarabu, tehran radio.
No comments
Post a Comment