Friday, 8 May 2015

Ajali ya Helikopta yauwa mabalozi Pakistan

Helikopta ya jeshi la Pakistan imeanguka leo na kuuwa watu saba iliokuwa ikiwasafirisha, wakiwemo mabalozi wa Norway na Ufilipino katika n... thumbnail 1 summary

Helikopta ya jeshi la Pakistan imeanguka leo na kuuwa watu saba iliokuwa ikiwasafirisha, wakiwemo mabalozi wa Norway na Ufilipino katika nchi hiyo. Kundi la Taliban nchini Pakistan limedai kuidungua helikopta hiyo likimlenga waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif, lakini maafisa wa Pakistan pamoja na walioishuhudia ajali hiyo wamekanusha madai hayo. Helikopta hiyo ilikuwa katika msafara uliozijumuisha nyingine mbili kuwasafirisha mabalozi katika ziara ya siku tatu katika jimbo la Gilgit Baltistan, ambako pia wangekutana na waziri mkuu Sharif. Ripoti ya jeshi la Pakistan na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje imesema ajali hiyo imetokana na hitilafu za kiufundi ilipokuwa ikitaka kutua.
Shule ambayo imeangukiwa na helikopta hiyo imefungwa. Mabalozi wa Poland na Uholanzi wamejeruhiwa katika ajali hiyo, ambayo pia imeuwa wake wa mabalozi wa Indonesia na Malaysia DW.

No comments

Post a Comment