Friday, 8 May 2015

Nkurunziza awasilisha fomu za kugombea mhula wa tatu

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewasilisha katika tume ya uchaguzi CENI fomu ya kugombea muhula wa tatu, ambao umezusha utata na kusab... thumbnail 1 summary
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewasilisha katika tume ya uchaguzi CENI fomu ya kugombea muhula wa tatu, ambao umezusha utata na kusababisha maandamano yenye umwagaji wa damu.
Nkurunziza amesema maandamano nchini mwake yamegeuka uasi, na kuahidi kuwa yatadhibitiwa hivi karibuni. Rais huyo pia ameahidi kwamba uchaguzi nchini mwake utakwenda vyema.
Vyama vya upinzani na mashirika ya kiraia vinasema mhula wa tatu kwa rais Nkurunziza unakiuka katiba ya nchi hiyo, lakini mahakama ya katiba ya nchi hiyo imemuidhinisha rais huyo kugombea tena.
Watu 18 wamekwishauawa tangu kuzuka kwa mzozo huo, na ripoti iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi, UNHCR, imesema watu 50,000 tayari wameondoka nchini Burundi na kukimbilia nchi jirani. Nkurunziza anakabiliwa na shinikizo kubwa la jumuiya ya kimataifa, kujiondoa katika uchaguzi wa rais utakaofanyika tarehe 26 Juni. DW

No comments

Post a Comment