Monday, 18 May 2015

Al Shabab wadai kukamata 'drone' ya Marekani Somalia

       Kundi la Al-Shabaab jana lilisema kuwa limekamata ndege moja isiyo na rubani ya Marekani iliyoanguka kwenye sehemu ya pwani ya Somali... thumbnail 1 summary
Al Shabab wadai kukamata 'drone' ya Marekani Somalia      Kundi la Al-Shabaab jana lilisema kuwa limekamata ndege moja isiyo na rubani ya Marekani iliyoanguka kwenye sehemu ya pwani ya Somalia.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Xhinhua la China, wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi walisema sasa wanamiliki ndege hiyo wanayodai kuwa ni ya Marekani, baada ya ndege hiyo kuanguka karibu na kijiji cha El Bashir.
Serikali ya Somalia au kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM zote hazijatoa maoni kuhusu habari hiyo. Marekani imetumia ndege zake zisizo na rubani kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi la Al-Shabaab, ambayo yamewaua viongozi kadhaa wa kundi hilo. Marekani hutekeleza hujuma kadhaa kutumia ndege zisizo na rubani nchini Somalia na pia katika nchi kama vile Pakistan, Yemen na Afghanistan. Kwa kawaida Marekani hudai kuwa inawalenga magaidi, hata hivyo raia wengi wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto  pia hupoteza maisha katika hujuma hizo.

No comments

Post a Comment