Makumi ya watu wamepoteza maisha kusini mwa Somalia baada ya mapigano makali baina ya magaidi wa kundi la al Shabaab na vikosi vya serikali.
Imearifiwa kuwa siku ya Ijumaa Al Shabaab walishambulia wanajeshi wa serikali katika kijiji cha Mubarak wilaya ya Awdheegle katika eneo la Lower Shabelle kusini mwa Mogadishu. Mapigano hayo yaliendelea hadi Jumamosi asubuhi. Wiki iliyopita pia kulijiri mapigano baina ya pande mbili hizo katika eneo hilo hilo. Msemaji wa kijeshi wa Al Shabaab Abdiasis Abu Musab amenukuliwa akidai kuwa kundi lake limewaua wanajeshi 25 wa serikali. Katika upande mwingine Abdikadir Mohammad Sidi, gavana wa Lower Shabelle amesema magaidi 40 wa kundi la Al Shabab wameuawa. Askari wa Umoja wa Afrika Somalia AMISOM wakishirikiana na wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuwatimua Al Shabaab kutoka maeneo mengi ya kusini mwa nchi hiyo. Hata hivyo magaidi hao waliokimbilia katika milima ya Galgala wangali wanatekeleza hujuma za kuvizia ndani ya Somalia kwenyewe na katika nchi jirani ya Kenya.
No comments
Post a Comment