Saturday, 23 May 2015

LOWASA AWEKWA HURU NA NEC

WAGOMBEA sita wa nafasi ya urais kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)waliotangaza nia kabla ya wakati wametolewa kifungoni kwa kutopewa adhabu... thumbnail 1 summary
WAGOMBEA sita wa nafasi ya urais kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM)waliotangaza nia kabla ya wakati wametolewa kifungoni kwa kutopewa adhabu yoyote na kuonywa kutorudia kitendo hicho kama wanataka kufikiriwa kuwania nafasi hiyo muda utakapofika.
Uamuzi huo ni wa Kamati Kuu ya CCM inayoendelea na vikao vyake mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete. Pia uamuzi huo umeondoa wingu kubwa lililotanda kwa wagombea urais wanaoonekana ni wenye mvuto kwenye chama hicho.
Nape Nnauye.
NAPE
Waliotolewa kwenye kifungo hicho ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Wengine ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira, Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamati kuu ilipokea na kutafakari taarifa ya kamati ya usalama na maadili na kuangalia adhabu ya wanachama sita waliokiuka maadili na kupewa adhabu kali na adhabu hiyo ilidumu kwa muda wa miezi 12.
Alisema pia Kamati Kuu: “Imepokea na kukubali pendekezo la kamati ya usalama na maadili ya kumalizika kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hao, kwa hiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika chama”.
Alisema Kamati Kuu imewataka wanachama wanaotaka kugombea urais kuzisoma, kuziheshimu na kuzingatia kanuni za maadili za CCM na michakato katika chama ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni.

No comments

Post a Comment