Tuesday, 19 May 2015

Bajeti ya ofisi ya Rais yapitishwa

Tue May 19 2015 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma CELINA KOMBANI Bunge limepitisha baje... thumbnail 1 summary
Tue May 19 2015
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma CELINA KOMBANI
Bunge limepitisha bajeti ya ofisi ya Rais na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Awali akiwasilisha bajeti ya Ofisi ya Rais na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma CELINA KOMBANI amesema kuwa zaidi ya ajira Elfu 70 zinatarajiwa kutolewa kwa kada mbalimbali katika mwaka wa fedha wa 2015/2016.

Waziri KOMBANI ameliambia bunge Mjini DODOMA kuwa kipaumbele katika ajira hizo kitaelekezwa katika sekta za Elimu na Afya.

Akiwasilisha makadirio ya matumizi ya ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Dakta MARY NAGU amesema kuwa mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano utalenga katika kujenga uchumi wa viwanda utakaopanua fursa ya ajira hasa kwa vijana.

Wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya Ofisi ya Rais na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha wa mwaka 2015/2016.

No comments

Post a Comment