Tue May 19 2015
Rais wa BURUNDI PIERRE NKURUZINZA
Rais wa BURUNDI PIERRE NKURUZINZA amewaonya wananchi wa nchi hiyo
kuchukua tahadhari kwakuwa kuna dalili ya kuvamiwa na kikundi cha
kigaidi cha AL SHABAAB
Akizungumza na waandishi wa habari katika IKULU ya nchi hiyo Rais NKURUZINZA amesema tishio hilo la kuvamiwa na magaidi si la BURUNDI pekee ni pamoja na nchi jirani za KENYA na UGANDA.
Wakati akitoa hotuba hiyo kwa waandishi wa habari rais huyo hakuzungumzia hali ya usalama inayoendelea nchini mwake wale waliotaka kuipindua serikali yake.
Wapinzani wa Rais PIERRE NKURUZINZA wameawataka wafuasi wao kujitokeza kwa wingi katika maandamano ya kumpinga rais huyo asigombee kwa awamu ya tatu nafasi ya urais.
Kufuatia hali ya sintofahamu inayoendelea nchini BURUNDI maelfu ya wananchi wan chi hiyo wameomba hifadhi katika nchi jirani huku watu kadhaa wakipoteza maisha katika maandamano na ghasia za kumpiga rais NKURUZINZA.
No comments
Post a Comment