Wednesday, 6 May 2015

BAN KI MON ASEMA DUNIA INAMWAMINI KIKWETE

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amesema dunia ina imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wengine wa Jopo la Watu M... thumbnail 1 summary
Katibu Mkuu wa Umoja wa Maaifa, Ban Ki-moon akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete katika ofisi yake jijini New York, Marekani ambapo Rais Kikwete aliongoza kikao cha kutafuta majawabu ya dunia kuhusu athari za magonjwa ya milipuko. (Picha na Freddy Maro).
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon amesema dunia ina imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wengine wa Jopo la Watu Maarufu Duniani waliopewa jukumu la kutafuta jinsi dunia inavyoweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko, kama vile ebola, katika siku zijazo.
Aidha, Ki-moon amewaambia wajumbe hao kuwa uteuzi wao uliofanywa na yeye mwenyewe mwezi uliopita umefanyika baada ya majina yao kuwa yamependekezwa na taasisi nyingine za kimataifa, mbali na Umoja wa Mataifa na ni matarajio yake kwamba jopo hilo litakuja na mapendekezo yanayolenga kuifanya dunia mahali bora zaidi pa kuishi.
Aliyasema hayo juzi wakati alipokutana na kuzungumza na wajumbe wa jopo hilo ofisini kwake katika Makao Makuu ya UN mjini New York, muda mfupi kabla ya wajumbe hao kufanya kikao chao cha kwanza chini ya uenyekiti wa Rais Kikwete.

No comments

Post a Comment