WIZARA ya Maliasili na Utalii imeomba kuongezewa muda wa kufanyia marekebisho maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii iliyotaka wizara hiyo kutekeleza maagizo, ikiwemo utekelezaji wa tozo mpya za viingilio kwenye hifadhi ya Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyeitikia mwito wa kufika mbele ya Kamati hiyo jana alisema kutokana na mwelekeo wa ratiba ya Bunge wizara ilitakiwa kufika mbele ya Kamati tena kama ilivyoagizwa juzi baada ya kutakiwa kwenda kufanya marekebisho ya ripoti yake, lakini kulingana na muda haikuwezekana kufanya marekebisho hayo kwa usiku moja, hivyo kuiomba kamati kuiongezea muda.
“Leo (jana) tumeitikia mwito wa Kamati wa kufika tena mbele ya kamati tukiwa tumefanya marekebisho, tumepokea hoja za kamati lakini tunaomba kupewa muda kuzifanyia kazi,” alisema.
Kutokana na ombi hilo, kamati hiyo ilitoa muda wa siku 10 hadi Mei 15, mwaka huu wizara hiyo iwe imefanya marekebisho ripoti yake na kuiwasilisha Dodoma ili Kamati iweze kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
No comments
Post a Comment