Tuesday, 5 May 2015

BEN CARSON atangaza kumrithi OBAMA Marekani laivulaivu

Tue May 05 2015 Daktari bingwa wa upasuaji na mwandishi wa vitabu maarufu, nchini MAREKANI, BEN CARSON Daktari bingwa ... thumbnail 1 summary
Tue May 05 2015
Daktari bingwa wa upasuaji na mwandishi wa vitabu maarufu, nchini MAREKANI, BEN CARSON
Daktari bingwa wa upasuaji na mwandishi wa vitabu maarufu, nchini MAREKANI, BEN CARSON, ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais nchini humo kwa tiketi ya chama cha Republican.

CARSON ambaye hivi sasa amestaafu, ametangaza kushiriki katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi mkuu wa MAREKANI unaotarajiwa kufanyika mwakani.

CARSON anakuwa ni raia wa MAREKANI wa kwanza mwenye asili ya AFRIKA kuweza kuingia katika kinyang’anyiro cha urais katika chama cha Republican.

CARSON, amejipatia umaarufu sana ndani ya nje ya nchi ya MAREKANI, kutokana na vitabu vyake viwili kikiwemo cha THINK BIG, vilivyoweza kubadilisha mtizamo na maisha ya watu mbalimbali duniani kuelekea kwenye maendeleo.

Daktari huyo pia amefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa kwa wagonjwa, ikiwemo kutenganisha mapacha waliokuwa wameungana kwenye fuvu la kichwa.

Wengine ambao tayari wametangaza ni ya kugombea kiti hicho mwakani, ni pamoja na HILLARY CLINTON.

No comments

Post a Comment