Tue May 05 2015
Kitukuu wa Malkia ELIZABETH wa uingereza apewa jina
Hatimaye kitukuu cha Malkia ELIZABETH, wa UINGEREZA kilichozaliwa
mwishoni mwa wiki iliyopita kimepata jina. Kitukuu hicho ambacho ni
mtoto wa WILLIAM na KATE, mjukuu wa Malkia, kimepatia jina la CHARLOTE
ELIZABETH DIANA.
Mtoto huyo wakifalme amepatiwa majina ya wanawake wa ukoo wa kifalme wa UINGEREZA, ambapo CHARLOTE, aliishi karne ya 18 na alijipatia umaarufu kwa kuzaa watoto wengi katika ukoo huo.
ELIZABETH ndiye malkia wa sasa na DIANA ni mama wa WILLIAM, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari na alikuwa akipendwa sana na raia wengi wa UINGEREZA kutokana na tabia yake ya kupenda watoto na kuwa na huruma kwa wenye shida.
Sherehe za kupewa jina mtoto wa kifalme zimeambatana na taratibu za kifalme za kupigwa kwa mizinga nje ya jengo la kifalme.
No comments
Post a Comment